Sunday, December 9, 2012
XAVI AMHUSUDU SCHOLES.
KIUNGO wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Xavi Hernandez amezungumzia jinsi anamhusudu kiungo wa Manchester United Paul Scholes akimuelezea kama mchezaji alikamilika na bora katika kipindi chake. Katika mahojiano ya mchezaji huyo na tovuti ya Daily Mail, Xavi amesema kuwa Scholes ni kiungo aliyekamilika na kama angekuwa anacheza La Liga yaani Ligi Kuu nchini Hispania angeheshimika zaidi tofauti na Uingereza. Amesema Uingereza ni taifa la mashujaa hivyo aina yao ya uchezaji ni tofauti na La Liga kwani ligi yao wanatumia nguvu sana na mchezaji anavyocheza kwa nguvu nyingi mashabiki humshangilia kitendo ambacho ni tofauti na Hispania ambapo mashabiki hupenda kuangalia soka la pasi nyingi na sio nguvu. Xavi aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miaka 15 hadi 20 iliyopita amekuwa ni mchezaji bora wa kati aliyekamilika ambaye amepata kumuona na mpaka sasa ameendelea kuonyesha ubora wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment