Sunday, December 30, 2012

RONALDINHO ATAMANI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2014.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Ronaldinho Gaucho ameeleza kuwa anahitaji kuwamo katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitashiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona ana matumaini kuwa atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michuano hiyo katika kipindi cha miezi 18 ijayo ambayo itaandaliwa nchini kwake. Ronaldinho amesema hakuna kitu kinacholeta furaha kama kucheza michuano ya Kombe la Dunia mbele ya mashabiki wa nyumbani na hapendi kupoteza nafasi hiyo muhimu. Kwasasa nyota huyo ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Atletico Mineiro amekuwa akipambana kurejesha makali yake ya zamani ili aweze kuitwa katika kikosi hicho na anaamini katika kipindi cha miezi 18 ijayo atakuwa amefikia kiwango hicho. Luiz Felipe Scolari ambaye ameisaidia Brazil kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 2002 wakati huo Ronaldinho akiwa ndio nyota nchi hiyo ndio amekabidhiwa tena mikoba ya kuinoa timu ya taifa Novemba.

No comments:

Post a Comment