Wednesday, December 12, 2012

SANTOS YAMTANGAZIA DAU ROBINHO.

RAIS wa klabu ya Santos ya Brazil Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amesema kuwa klabu yake hiyo imetangaza dau kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya AC Milan ya Italia Robinho na kumrejesha nyumbani katika klabu ambayo ndio alianza kucheza soka. Ribeiro amekiri kuwa dau hilo walilotoa limeonekana ni dogo kwa mahitaji ya mchezaji huyo mwenye miaka 28 pamoja na Milan lakini hiyo ni hatua ya kwanza katika mbio za kutaka kumrejesha nyumbani Robinho ambaye ameshinda mataji mawili ya ligi akiwa na timu hiyo mwaka 2002 na 2004. Rais huyo amesema kuwa tayari wameshatuma barua rasmi kwa Milan na anaamini kuwa watafikia makubaliano mwishoni kwani Robinho ameonyesha nia ya kutaka kurejea nyumbani baada ya kucheza Ulaya kwa kipindi kirefu. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil pia aliwahi kucheza katika vilabu vya Real Madrid ya Hispania kuanzia mwaka 2005 mpaka 2008 na kutimkia Uingereza katika klabu ya Manchester City ambayo aliondoka mwaka 2010 na kwenda Milan. 

No comments:

Post a Comment