Wednesday, December 12, 2012

FERGUSON AMNYATIA WALCOTT.

KLABU ya Manchester United imeingia katika kinyang’anyiro cha kumgombea winga wa Arsenal Theo Walcott kama walivyofanya wakati walipomchukua Robin van Persie Agosti mwaka huu. Meneja wa United Sir Alex Ferguson amenuia kumchukua winga huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye mkataba wake unaishia mwishoni mwa msimu huu. Walcott akama ilivyokuwa kwa Van Persie amekataa kusaini mkataba mpya mpya ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 75,000 kwa wiki na kudai kuwa kama klabu hiyo inamuhitaji basi haina budi kumlipa paundi 100,000 kwa wiki. Liverpool, Manchester City na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kumsajili winga huyo lakini United ndio wanaonekana wana nafasi kubwa ya kumnyakuwa baada ya Walcott mwenyewe kuonyesha kuvutiwa na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment