Wednesday, December 12, 2012

WENGER AKATAA KUWALAUMU WACHEZAJI WAKE BAADA YA KUTOLEWA BRADFORD.

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amewatetea wachezaji wake baada ya kutolewa na Bradford City kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo war obo fainali ya Kombe la Ligi lakini amekiri kuwa tatizo la umaliziaji nalo lilichangia kupoteza mchezo huo. Arsenal ilitolewa kwa kufungwa matuta 3-2 baada ya wachezaji watatu wa timu hiyo kukosa penati na kocha huyo raia raia wa Ufaransa analaumu uwezo wa wachezaji wake kutumia nafasi walizopata kuwa ndio chanzo kikubwa cha kufungwa. Akiohijiwa mara baada ya mchezo huo Wenger huo Wenger amewasifu wapinzani wao  Bradford kwa kuanza mchezo vyema na kupata bao la mapema halafu kwa kuwadhibiti vyema washambuliaji wake ili wasilete madhara langoni kwao. Wenger alikataa kuwalaumu wachezaji wake kwa kucheza chini ya kiwango kwani walipata wakati mgumu kutokana na Bradford kuzuia karibu muda wote wa mchezo huo hivy kuwapa wakati mgumu wapinzani wao kuwafunga. Kombe la Ligi ndio pekee Arsenal ilikuwa ikipewa nafasi ya kulinyakuwa ili kukata kiu ya miaka saba ya kukosa taji lolote lakini bado wana nafasi nyingine katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo wameingia katika hatua ya timu 16 bora.

No comments:

Post a Comment