Wednesday, December 5, 2012

SHEHATA ATUPIWA VIRAGO BAADA YA KUFUNDISHA MIEZI MWILI NCHINI QATAR.

KLABU ya Al Arbi ya Qatar imemtupia virago vyake kocha wa zamani wa Misri Hassan Shehata baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa kipindi cha miezi miwili pekee. Klabu hiyo ilitangaza kusitisha mkataba na Shehata kutokana na matokeo mabao iliyopata timu hiyo katika michezo yake ya Ligi Kuu nchini humo. Akihojiwa na televisheni ya Qatar Shehata amesema kuwa ameshangazwa na uamuzi uliochukuliwa na klabu hiyo ingawa kwa upande mwingine anashukuru kuondoka kwani alifanya kila awezalo lakini wachezaji wameshindwa kujisaidia. Shehata aliendelea kusema kuwa kuanza sasa atakuwa hakubali kazi yoyote ya kufundisha timu mpaka aifanyie uchunguzi klabu husika yasije kumkuta kama yaliyomkuta Al Arbi. Klabu hiyo sasa inashika mkia katika msimamo wa ligi nchini humo wakiwa wamejikusanyia alama nne pekee.

No comments:

Post a Comment