Wednesday, December 5, 2012

SINA MUDA WA KUPUMZIKA - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho amesema kuwa hatakuwa na muda wa kupumzika wakati akiamua kuondoka katika klabu hiyo. Kumekuwa na tetesi kuwa Mourinho ambaye ni raia wa Ureno ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huku taarifa hizo zikielekeza kuwa kocha huyo atakwenda katika klabu za Manchester City au Paris Saint-Germain. Lakini kocha huyo wa zamani wa klabu za Porto, Chelsea na Inter Milan amesema kuwa kama ataondoka Santiago Bernabeu anatarajia haraka kutafuta timu nyingine na sio kupumzika. Mourinho amesema hatachukua likizo ya mwaka mzima kwa akiondoka Hispania ataelekea kokote kule kuendelea kufundisha. Madrid kwasasa inashika nafasi ya tatu katika La Liga wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo Barcelona kwa alama 11 huku wakiwa wamepitwa lama tano na mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment