Wednesday, December 5, 2012
CAF REVEALS TOP THREE.
SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetaja majina matatu ya mwisho ya wachezaji watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2012. Nyota wa Ivory Coast Yaya Toure ambaye anashikilia tuzo ya mwaka jana na Didier Drogba ambaye ameshinda tuzo hiyo mwaka 2006 na 2009 watakuwa wakipambana na kiungo wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Barcelona Alexander Song. Kwa upande wa orodha ya mwisho ya wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika wachezaji wa Zambia Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu ambao wote wanacheza katika klabu ya TP Mazembe ya DRC na Mohamed Abou Trika wa Misri na klabu ya Al Ahly ndio watakaogombea tuzo hiyo. Mshindi katika tuzo hizo atatangazwa katika sherehe zitakazofanyika jijini Accra, Ghana Desemba 20 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment