Wednesday, December 5, 2012

MESSI HATIHATI KUIKOSA REAL BETIS.

KLABU ya Barcelona imesema kuwa mshambuliaji wake nyota Lionel Messi amepata majeruhi ya goti lake la kushoto na kuna hatihati akakosekana katika wa La Liga dhidi ya Real Betis unaotarajiwa kuchezwa Jumapili. Katika taarifa iliyotumwa katika tovuti ya klabu hiyo imesema vipimo alivyofanyiwa nyota huyo vimethibitisha kuwa amepata mchubuko katika mfupa wa goti lake na kupona kwake kutakuwa taratibu hivyo kuwepo uwezekano mkubwa wa kukosa mchezo huo. Mchezaji huyo bora wa dunia aliondolewa katika machela katika mwishoni mwa mchezo wa kundi G wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Benfica baada ya kugongana na golikipa wa timu hiyo wakati akijaribu kufunga. Pamoja na sare ya bila kufungana iliyopata Barcelona katika mchezo huo walikuwa tayari wamefuzu katika hatua ya timu 16 bora wakiwa vinara wa kundi lao huku wapinzani wao Benfica wakishindwa kusonga mbele na kupata nafasi katika Europa League. Messi amebakisha bao moja ili kufikia rekodi ya mabao 85 aliyoweka Gerd Muller katika kipindi cha mwaka mmoja, hiiyo ikiwa mwaka 1972.

No comments:

Post a Comment