Thursday, December 20, 2012

SINA MAJIVUNO - RONALDO.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid , Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa hana majivuno kama vyombo vya habari vinavyodai. Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akishutumiwa kukosa ubinadamu kulinganisha na nyota wa Barcelona Lionel Messi na baadhi ya vyombo vya habari nchini Hispania. Hatahivyo suala hilo limeonekana kutomsumbua Ronaldo ambaye ameelezea furaha yake ya kuwa na familia ambayo imemfanya kutulia na kuwa mchezaji wa kiwango cha juu na aliyekomaa. Ronaldo amesema pindi awapo uwanjani huwa mchezaji ambaye hufanya vitu kwa umakini na huwa hapendi kucheka mara kwa mara na hilo ndio tatizo watu wanadhani pengine ana dharau lakini sivyo wanafikiria hata kidogo. Nyota huyo aliongeza pia anapenda kuongeza mtoto mwingine kwani kuwa na familia kubwa ni kitu anachokipenda.

No comments:

Post a Comment