Thursday, December 20, 2012

MBINU MBAYA ZA UFUNDISHAJI WA MOURINHO NDIO ZINAIYUMBISHA MADRID KWASASA.

NGULI wa zamani wa klabu ya Barcelona, Johan Cruyff amedai kuwa klabu ya Real Madrid inayumba kwasasa`kutokana na mbinu za ufundishaji za meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho. Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga wamekuwa wakisuasua katika wiki za karibuni na Cruyff ambaye ni raia wa Uholanzi anadhani kuwa klabu hiyo ingefanya vizuri kama ingekuwa inavuna wachezaji katika shule yake ya soka. Cruyff amesema tabia hasi aliyonayo Mourinho lazima iwe na madhara kwani anadhani mbinu anazotumia kufundisha ziko sawa kutokana na matokeo ya nyuma lakini yeye anaamini haziko sawa. Amesema hashangazwi na yanayotokea klabuni hapo hivi sasa kwani vitu kama hivyo hutokea wakati falsafa yako ni kusaini na kutegemea majina makubwa badala ya wachezaji uliowatengeneza mwenyewe. Cruyff alimalizia kuwa kikosi cha Barcelona ambacho kitamkosa kocha wake Tito Vilanova aliyefanyiwa upasuaji wa koo ili kondoa uvimbe wa kansa kwa kipindi cha miaezi mitatu mpaka minne kitaendelea kufanya vizuri pamoja na kutokuwepo kwa kocha wao huyo.

No comments:

Post a Comment