Thursday, December 20, 2012

UPASUAJI WA VILANOVA WAFANIKIWA.

KLABU ya Barcelona imesema kuwa upasuaji wa koo aliofanyiwa meneja wake Tito Vilanova umemalizika salama na kocha huyo anaendelea vyema. Klabu hiyo ilitangaza Jumatano kuwa Vilanova alikuwa akihitaji uapsuaji wa pili baada ya kufanyiwa upasuaji mara ya kwanza kuondoa Novemba mwaka 2011. Katika taarifa iliyotumwa katika tovuti ya klabu hiyo imesema Vilanova anatarajiwa kubakia hospitalini kwa kipindi cha siku tatu mpaka nne na baada ya hapo atakuwa akiendelea na matibabu ya mionzi. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 alipumzika kwa kipindi cha wiki baada ya kufanyiwa upasuaji mwaka jana kabla ya kurejea tena katika kazi yake kama msaidizi wa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola. Kikosi cha Barcelona ambacho kwasasa ndio kinaongoza Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga kitakuwa chini ya kocha msaidizi Jordi Roura mpaka hapo Vilanova atakaporejea tena baada ya kupona.

No comments:

Post a Comment