Thursday, December 20, 2012

ARSENAL, BAYERN MUNICH ZOTE ZINA NAFASI YA KUTINGA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE - PODOLSKI.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Lukas Podolski anaamini kuwa klabu yake hiyo ina nafasi kubwa ya kusonga katika hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupangwa na mabingwa wa zamani wa michuano hiyo Bayern Munich. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alicheza katika klabu hiyo kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2006 mpaka 2009 kabla ya kurejea klabu ya nyumbani kwao ya Koln. Podolski amekiri kuwa hautakuwa mchezo rahisi kutokana na ubora na uzoefu wa Bayern Munich katika michuano hiyo lakini anaamini kuwa timu zote mbili zina nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali. Bayern ilifungwa katika mchezo wa fainali na Chelsea May mwaka jana na pia walipoteza mchezo dhidi ya Inter Milan katika hatua kama hiyo mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment