Thursday, December 20, 2012

YAYA TOURE MCHEZAJI BORA WA MWAKA.

KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City, Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa mara ya pili mfululizo na kumpita mwenzake ambaye wanatoka nchi moja Didier Drogba. Toure mwenye umri wa miaka 29 alipata kura nyingi zaidi za makocha wa timu za taifa pamoja na wakurugenzi wa benchi la ufundi na kushinda tuzo hiyo ambayo pia aliinyakuwa mwaka 2011. Nyota huyo alikuwa akifuatiwa kwa karibu na Drogba ambaye aliisaidia klabu yake ya zamani Chelsea kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga penati ya ushindi huku Toure yeye akiwa ameisaidia Ivory Coast katika michuano ya Mataifa ya Afrika pamoja na kuisaidia klabu yake kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya miaka 35. Mbali na Toure wengine waliopata tuzo katika sherehe hizo zilizofanyika jijini Accra, Ghana ni pamoja na Mohammed Abou Trika alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa Afrika, Genoveva Anomna wa Equatorial Guinea alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanawake. Mabingwa wa Afrika Zambia ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka huku kocha wake Herve Renard naye akitunukiwa tuzo ya kocha bora wa mwaka na tuzo ya klabu bora ya mwaka ilikwenda kwa mabingwa wa Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika Al Ahly.

No comments:

Post a Comment