Sunday, December 23, 2012

SIJIUZULU NG'O - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho amesisitiza kuwa hatajiuzulu wadhfa huo pamoja na timu yake kufungwa mabao 3-2 na Malaga ambao umewafanya kuachwa alama 16 na vinara wa La Liga Barcelona. Kufungwa kwa Madrid kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Mourinho kufuatia uamuzi wake wa kumuacha golikipa ambaye ndiye nahodha wa timu hiyo Iker Casillas katika kikosi cha kwanza. Akihojiwa kama anahofu kibarua chake kitakuwa kimefikia ukingoni mara baada ya mchezo Mourinho amesema hahofii chochote na hawezi kuachia ngazi kwani kupoteza mechi ni sehemu ya mchezo la msingi ni kujipanga na kuangalia wapi walikosea. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Casillas katika kipindi cha miaka 10 kupumzishwa benchi na kumpisha golikipa namba mbili Antonio Adan mwenye umri wa miaka 25.

No comments:

Post a Comment