Sunday, December 23, 2012

VILANOVA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.

MENEJA wa Barcelona, Tito Vilanova ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa upauji kuondoa uvimbe wa kansa uliokuwa umeota kwenye koo. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alifanyiwa upasuaji huo Alhamisi iliyopita na kwasasa anakabiliwa na matibabu ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita ili kudhibiti kabisa tatizo hilo linalomkabili. Huo ni upasuaji wa pili kufanyiwa baada ya ule aliofanyiwa mwaka 2011 kipindi hicho akiwa msaidizi wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pep Guardiola. Barcelona ilifanikiwa kuifunga Valladolid mabao 3-1 jana usiku na baada ya hapo Xavi Hernandez ambaye alifunga bao la kwanza amesema wanamzawadia ushindi huo kocha wao huo ambaye anapitia kipindi kigumu hivi sasa katika maisha yake. Kwasasa kocha msaidizi Jordi Roura ambaye amekuwa benchi la ufundi la klabu hiyo toka mwaka 2009 ndiye aliyekabidhiwa timu wakati wa kipindi hiki ambacho Vilanova hayupo.

No comments:

Post a Comment