Sunday, December 9, 2012

SUPER FALCONS YANGOZA ORODHA ZA AFRIKA.

KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya wanawake wa Nigeria-Super Falcons, Rita Nwadike amesema kuwa hakushangazwa na kushika nafasi ya kwanza katika orodha za ubora kwa upande wa Afrika zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. FIFA ilitaja orodha hizo za mwisho wa mwaka Ijumaa na kuiweka Nigeria katika nafasi ya kwanza kwa upande wa Afrika na 32 duniani ikifuatiwa na Cameroon katika nafasi ya pili, Ghana katika nafasi ya tatu wakati mabingwa wa Afrika mwaka huu Equatorial Guinea wakiwa katika nafasi ya nne. Nchi zingine zilizotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Afrika Kusini ambao wako katika nafasi ya tano, Ivory Coast nafasi ya sita, Morocco nafasi ya saba, Tunisia nafasi ya nane, Algeria nafasi ya tisa, Misri nafasi ya 10, Senegal nafasi ya 11, Mali nafasi ya 12, Zimbabwe nafasi ya 13 na Ethiopia katika nafasi ya 14. Nwadike amesema kuwa hakushangazwa na kitendo cha FIFA kuwapa nafasi ya kwanza kwa upande wa bara la Afrika kwani walikuwa wakifahamu hilo pamoja na kupoteza taji la ubingwa wa Afrika nchini Equatorial Guinea. Kocha huyo aliendelea usema kuwa mabingwa wa sasa michuano hiyo ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano hiyo Equatorial Guinea timu yao imeundwa na wachezaji wengi kutoka Brazil na Nigeria na sio wazawa halisi wa nchi hiyo. Orodha nyingine ya FIFA kwa upande wa wanawake itatolewa Machi 22 mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment