Thursday, December 6, 2012

GOAL LINE TEKNOLOGY YAANZA KUTUMIKA RASMI JAPAN.

TIMU ya Sanfrence Hiroshima ya Japan imeifunga timu ya Auckland City ya New Zealand kwa bao moja kwa bila katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia jana ambao Shrikisho la Soka Dunia-FIFA lilitumia mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli kwa mara ya kwanza. Bao Hiroshima lilifungwa dakika ya 66 na Toshihiro Aoyama na kuwapeleka mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Japan maarufu kama J-League katika hatua ya robo fainali ambapo sasa watakwaanza na mabingwa wa soka barani Afrika Al Ahly ya Misri. Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa FIFA kutumia rasmi mfumo huo ingawa kulikuwa na nafasi finyu za kujaribu ubora wake kutokana na mchezo wenyewe uliokuwa na nafasi chache za kufunga. FIFA inatumia mifumo katika viwanja vilivyopo katika miji ya Yokohama na Toyota ambapo kunafanyika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment