Thursday, December 6, 2012

OBI MIKEL AFUNGIWA MECHI TATU.

KIUNGO wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya Chelsea, John Obi Mikel amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya paundi 60,000 baada ya kukwaruzana na mwamuzi aliyechezesha mchezo baina ya timu hiyo Manchester United. Mikel aliripotiwa kuwa alivamia chumba cha waamuzi baada ya mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge Octoba mwaka huu kufuatia tuhuma kwamba Mwamuzi Mark Clattenburg alishambulia kiungo huyo kwa maneno ya kibaguzi. Chama cha Soka cha Uingereza-FA kimesema kuwa nyota huyo alikiri kutumia maneno ya kutishia katika chumba cha waamuzi mwishoni mwa mchezo huo uliochezwa Octoba 28 ambapo Chelsea walipoteza kwa kufungwa mabao 3-2. Adhabu hiyo itapelekea nyota huyo kukaa nje uwanja mpaka Desemba 26 mwaka huu kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu ya nchi hiyo pekee lakini atakuwemo katika kikosi kitakachoelekea Japan kwajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.

No comments:

Post a Comment