Thursday, December 6, 2012

EURO 2020 KUFANYIKA ACROSS EUROPE.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Gianni Infantino amesema kuwa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo imekubali michuano ya Ulaya ya 2020 kuchezwa katika bara zima. Nahodha wa zamani wa Ufaransa, Michel Platini ambaye ni rais wa UEFA ndio aliyetoa wazo la michuano hiyo kuandaliwa na nchi nyingi zaidi mapema mwaka huu ikiwa ni njia ya kupunguza gharama za maandalizi haswa katika kipindi hiki ambacho nchi nyingi zimekuwa zikikumbwa na matatizo ya midororo ya kiuchumi. Infantino amesema michuano ya Euro 2020 itaandaliwa katika miji mbalimbali mikubwa kufuatia uamuzi uliotolewa na kamati hiyo jana. Taarifa za michuano hiyo kuandaliwa katika miji miji mikubwa tofauti haijapokewa vizuri na mashabiki wa soka wakidai gharama za kwenda kutizama timu zao kutoka nchi moja kwenda nyingine zitakuwa kubwa tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo mashabiki husafiri katika nchi moja au mbili ili kushuhudia michuano hiyo. Lakini wakati mashabiki wakilalama gharama za usafiri mashirika ya ndege barani humo yamefurahia habari hiyo kwani ndio utakuwa wakati wa kupata abiria wengi watakaokuwa wakienda katika miji ambayo itakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment