SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limemuongezea adhabu beki wa kimataifa wa Malta Kevin Sammut kutoka miaka 10 mpaka kumfungia maisha kujishughulisha na masuala ya soka baada ya kukutwa na hatia ya kupanga matokeo. Mchezaji huyo alikutwa na hatia ya kupanga matokeo katika mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2008 kati ya Norway na Malta ambapo katika mchezo huo nchi yake ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0. Agosti mwaka huu kamati ya nidhamu ya UEFA ilimfungia miaka 10 lakini mchezaji huyo na mkaguzi wa kamati hiyo walikata rufani kutaka adhabu hiyo iangaliwe upya ndipo adhabu ya kufungiwa maisha ilipotolewa. Sammut amepewa siku 10 za kukata rufani katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kupinga adhabu hiyo aliyopewa.
No comments:
Post a Comment