Monday, December 3, 2012

UHALIFU HUPUNGUA PINDI CHICHARITO ANAPOKUWA AKICHEZA - POLISI.

NYOTA wa kimataifa wa Mexico na klabu ya Manchester United, Juvier Hernandez amekuwa maarufu nchini kwake mpaka kufikia hatua ya matukio ya uhalifu kupungua pindi anapocheza. Mbali na uhalifu kupungua lakini wanawake wajawazito wanaokaribia kujifungua nao hushikwa na uchungu kwa furaha pindi nyota huyo anapoifungia bao timu yake ya United hivyo idadi ya watoto kuzaliwa kuongezeka. Ofisa wa juu wa polisi wa mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City, Jorge Carlos Martinez amesema kuwa uhalifu kama wa kuteka magari, uvamizi na ukabaji hupungua na inavyoonekana wahalifu hutumia muda huo kumuona shujaa wao wakati anacheza. Ofisa huyo wa polisi amesema kuwa ana matumaini meneja wa United Sir Alex Ferguson ataendelea kumtumia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 wakati wa kipindi hiki ambacho mji huo unakumbwa na matukio mengi ya uhalifu. Watu zaidi ya 15,000 huuliwa kila mwaka na magenge ya wauza madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment