Monday, December 3, 2012

CECAFA TUSKER CUP: KILIMANJARO STARS USO KWA USO NA ZANZIBAR HEROES NUSU FAINALI.

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Cecafa Tusker Cup kwa kuifunga Rwanda kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa KCC uliopo eneo la Lugogo, Kampala Uganda. Katika mchezo huo ambao vijana wa Kilimanjaro walionyesha ufundi mkubwa na kuwafunika kabisa Rwanda walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 33 bao ambalo lilifungwa na kiungo Amri Kiemba baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Mwinyi Kazimoto. Bao hilo lilionyesha kuamsha ari ushindi wa ambapo Kilimanjaro waliongeza kasi ya mashambulizi na kukosa mabao kadhaa kabla ya timu hizo hazijakwenda mapumziko Rwanda au Amavubi wakiwa vichwa chini kwa kuwa nyuma kwa bao moja. Vijana wa Kilimanjaro ambao wananolewa na kocha Kim Poulsen walianza kupindi cha kwa kasi kubwa na kuenyesha hawakutosheka na bao walilopata katika kipindi cha na juhudi zao hizo zilizaa matunda dakika ya 55 baada ya John Bocco kufunga bao la pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa baada ya kushindwa kumudu kunyaka shuti kali la Kazimoto. Kikosi cha Amavubi ambacho kilikuwa kikiongozwa na nahodha wake Haruna Niyonzima katika mchezo wa leo hakikuonyesha kuwa na madhara sana kwa vijana wa Kilimanjaro baada ya kubanwa kila idara. Katika robo fainali nyingine Zanzibar Heroes nayo ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Burundi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5 baada ya timu hizo kutoka sare ya bila ya kufungana katika muda wa kawaida. Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Zanzibar Heroes watakutana na ndugu zao Kilimanjaro Stars katika nusu fainali ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment