Tuesday, December 4, 2012

WENGER AWEKA WANNE KATIKA RADA ZAKE JANUARI.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anajipanga kumsajili mpachika mabao wa klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani Klaas-Jan Huntelaar mwezi ujao katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kwa ada ya paundi milioni sita. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akitazamwa kwa karibu na maskauti wa klabu hiyo wakati wa wiki za ufunguzi wa msimu mpya.  Wenger amekuwa akimhitaji nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa kipindi kirefu na baada ya kushauriana na mkuu wa maskauti wa klabu hiyo kocha huyo ameamua kumfukuzia nyota huyo mara dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa. Mbali na mchezaji huyo Wenger pia anapanga kumchukua tena kwa mkopo Thierry Henry na kumtengea kitita cha paundi milioni tisa kinda lenye maajabu la Crystal Palace, Wilfried Zaha. Arsenal pia iko sokoni ikitafuta golikipa mpya huku Pepe Reina akitajwa kuwa chaguo la kwanza la Wenger.

No comments:

Post a Comment