KATIKA kusheherekea tuzo ya nne ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or aliyopewa Lionel Messi Kampuni ya Adidas imempa mshambuliaji huyo wa Barcelona kiatu maalumu aina ya Adizero F50 kwa ajili ya tuzo hizo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye aliwapiku mchezaji mwenzake wa Barcelona Andres Iniesta na Criastiano Ronaldo wa Real Madrid, amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hizo mara nne mfululizo baada ya kufunga mabao 91 mwaka jana.
Viatu hivyo maalumu vilivyotolewa na Adidas vinaonyesha miaka yote ambayo Messi ameshinda Ballon d’Or ikiwa ndani ya nembo ya taifa ya Argentina inayojulikana kama Sun of May. Itakuwa ngumu kwa mtu wa kawaida kupata kununua kiatu hicho kwani kampuni hiyo haina mpango wa kutoa viatu zaidi vya aina hiyo kwa watu wengine.
No comments:
Post a Comment