Sunday, January 13, 2013

DZEKO MGUU NDANI MGUU NJE CITY.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Edin Dzeko ameonyesha nia yake ya kurejea katika Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Manchester City. Dzeko amefunga mabao sita msimu huu akitokea benchi na kuna taarifa kuwa mchezaji huyo hafurahishwi kuwepo katika klabu hiyo na hivyo yuko tayari kusikiliza ofa kutoka katika timu yoyote kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili. Nyota huyo amesema kila kitu kinawezekana hivyo anaweza kuondoka kuondoka kipindi hiki au katika majira ya kiangazi lakini kwasasa anajaribu kutofikiria hilo na kujaribu kutumia nafasi anayopewa na City. Mbali na mchezaji huyo pia kumekuwa na tetesi za kuondoka kwa mshambuliaji mwingine nyota wa klabu Sergio Aguero lakini taarifa hizo zilikanushwa na mchezaji mwenzake Pablo Zabaleta ambaye alidai kuwa nyota huyo anafurahia maisha katika klabu hiyo na hama mpango wa kuondoka.

No comments:

Post a Comment