Wednesday, January 2, 2013

NIERSBACH ATAKA MKATABA WA LOEW KUSHUGHULIKIWA HARAKA.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Ujerumani-DBF, Wolfgang Niersbach amesema anataka kumaliza haraka suala la mkataba wa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Joachim Loew kabla ya michuano ya Kombe la Dunia mwakani itakayofanyika nchini Brazil. Niersbach amesema atakereka kama suala la Loew halitatatuliwa mpaka kuelekea katika michuano hiyo. Loew ambaye aliteuliwa kukinoa kikosi cha nchi hiyo baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2006 ana mkataba ambao unamalizika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014. Hatahivyo Loew mwenye umri wa miaka 52 ameonyesha hana haraka juu ya mazungumzo ya kuongeza mkataba na kudai kuwa suala muhimu ni kuhakikisha nchi hiyo inafuzu Kombe la Dunia kwanza ndipo waanze mazungumzo.

No comments:

Post a Comment