Wednesday, January 2, 2013

TOTTENHAM BADO YASUBIRIA UAMUZI WA ADEBAYOR.

KLABU ya Tottenham Hotspurs bado haijakuwa na uhakika kama mshambuliaji wake nyota Emmanuel Adebayor ataamua kuungana na timu yake ya taifa ya Togo kwa ajili ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Kama nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ataamua kushiriki katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19 anaweza kukosa michezo mitano ya Ligi Kuu nchini Uingereza. Adebayor aliisaidia Spurs kupata ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo dhidi ya Reading uliofanyika jana na kuondoka kwake itakuwa pigo kubwa kwa klabu hiyo. Lakini meneja wa Spurs, Andre Villas-Boas amesema kuwa kamanyota huyo ataamua kuondoka kujiunga na nchi yake wataheshimu uamuzi wake. Adebayor alisusia michezo ya kimataifa kulishinikiza Shirikisho la Soka nchini Togo kutoa marupurupu ambayo wamekuwa wakicheleweshewa katika mechi kadhaa zilizopita.

No comments:

Post a Comment