Tuesday, January 1, 2013

NITAPIGANIA NAMBA YANGU - CASILLAS.

NAHODHA wa klabu ya Real Madrid, Iker Casillas amesisitiza kuwa ameongeza muda wa kujifua mazoezini ili aweze`kupata namba tena katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Casillas mwenye umri wa miaka 31 alienguliwa katika kikosi cha kwanza wakati Madrid ilipokubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Malaga na kocha wake Jose Mourinho na nafasi yake kuchukuliwa na golikipa namba mbili Antonio Adan. Hatahivyo akiongea na waandishi wa habari baada ya mazoezi ya kwanza ya Madrid baada ya mapumziko ya kipindi cha baridi, golikipa huyo amesema anajitahidi kufanya kila awezalo ili aweze kupigania namba yake katika kikosi cha kwanza. Casillas amesema kocha ndio mwenye maamuzi ya kuamua nani acheze na asicheze katika mchezo unaofuata na wote wanamuunga mkono Mourinho na wana imani naye kwa maamuzi atakayochukua. Madrid kwasasa iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga kwa tofauti ya alama 16 na mahasimu wao Barcelona ambao wanaongoza msimamo wa ligi hiyo. 

No comments:

Post a Comment