Tuesday, January 1, 2013

WENGER ACHOMOA KUMREJESHA HENRY EMIRATES.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameondoa uwezekano wa kumsajili tena kwa mkopo mshambuliaji nyota wa zamani wa klabu hiyo Thierry Henry. Henry mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo ili kujiweka katika hali nzuri kufuatia kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu nchini Marekani-MLS akiwa na na timu ya New York Red Bulls. Wenger amesema nyota huyo hayuko fiti kwasababu ndio kwanza amerejea kutoka mapumzikoni hivyo kwasasa suala la kumsajili halipo. Henry alirejea katika klabu yake hiyo ya zamani mwaka 2011 baada ya kuondoka mwaka 2007 na kujiunga na Barcelona na kufunga bao pekee katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Leeds United.

No comments:

Post a Comment