Sunday, December 30, 2012

MILANOV MCHEZAJI BORA WA MWAKA BULGARIA.

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini Bulgaria-PFC kimemteua mshambuliaji wa klabu ya Litex Lovech, Georgi Milanov kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo mbele ya wachezaji wengine nyota akiwemo Dimitar Berbatov anayecheza katika klabu ya Fulham ya Uingereza. Milanov mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni mchezaji mdogo kuwahi kushinda tuzo hiyo na mchezaji wa kwanza ambaye anacheza soka chini humo kushinda tuzo hiyo toka mwaka 2001. Kiungo huyo amefunga mabao nane katika michezo 14 aliyocheza na kuwa mhimili wa kuisaidia klabu yake kukwea mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo. Akihojiwa mara baada ya sherehe hizo nyota huyo amesema ni heshima kubwa kwake kupokea tuzo huyo na kuwashukuru waandaji, wachezaji wenzake pamoja na kocha wake Hristo Stoichkov kwa kumsaidia kufikia kiwango alichonacho hivi sasa.

No comments:

Post a Comment