Monday, January 21, 2013
RAIS AWATEMBELEA CHIPOLOPOLO.
RAIS wa Zambia Michael Sata amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo kuwachaza wapinzani wao watakaokutana wakati watapoanza kampeni ya kutetea taji lao la michuano ya Mataifa ya Afrika baadaye leo. Rais huyo amewaambia wachezaji hao kuwa inabidi waweke katika mawazo yao watu wote wa Zambia wa nyuma yao hivyo watapoanza kampeni zao inabidi wapambane kama wapigania uhuru ili waweze`kuhakikisha wanarudi na kombe lao nyumbani. Rais Sata aliongozana na mkewe Dr Christine Kaseba, Waziri wa Michezo Chishimba Kambwili na maofisa wengine wa ngazi za juu wan chi hiyo wakati walipoitembelea Chipolopolo katika kambi yao nchini Afrika Kusini. Sata alikaribishwa na rais wa Shirikisho la Soka la Zambia Kalusha Bwalya, wajumbe wa kamati ya utendaji wa shirikisho hilo pamoja na viongozi wa jimbo la Mpumalanga ambao ndio wenyeji wao huko. Zambia inatarajia kuanza kampeni zake kwa kukwaana na Ethiopia katika Uwanja wa Mbombela jioni hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment