Saturday, January 19, 2013

TAARABT ACHAGUA KLABU BADALA YA TIMU YAKE YA TAIFA.

KIUNGO wa kimataifa wa Morocco na klabu ya Queens Park Rangers-QPR, Adel Taarabt amebainisha kuwa alikataa kuichezea timu yake ya taifa katika michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon na kuiacha klabu yake ambayo iko mkiani katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Akihojiwa Taarabt amesema kuwa klabu yake iko mkiani katika ligi hivyo hawezi kuiacha na kwenda kucheza Afcon na alizungumzaq na familia yake pamoja na marafiki wa karibu walikubaliana na uamuzi aliochukua. Nyota huyo aliendelea kusema anajua mashabiki wa soka wa nchini kwake wamekasirishwa na uamuzi huo lakini Morocco ina wachezaji wazuri hata kama yeye hayupo wanaweza kufanya vizuri. Hivi karibuni kiungo huyo aliingia katika mzozo na Shirikisho la Soka la Morocco baada ya kumtaka kuomba radhi kwa maandishi kwa tuhuma za kumvunjia heshima kocha wa kikosi cha timu ya taifa Rachid Taoussi.

No comments:

Post a Comment