MAHAKAMA Usuluhishi wa Migogoro ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imewataka mchezaji wa kimataifa wa Guinea, Ismael Bangoura na klabu yake ya Nantes ya Ufaransa kuilipa klabu ya Al Nasr kiasi cha euro milioni 4.5 kama fidia kwa kuvunja mwkaubaliano ya mkataba. Mchezaji huyo alihamia nchini Ufaransa mwaka jana lakini sasa inaonekana kuwa uhamisho huo ulienda kinyume na makubaliano na klabu ya Al Nasr yenye maskani yake jijini Dubai. Mbali na kutakiwa kulipa faini hiyo, Nantes watatakiwa kutosajili mchezaji yoyote mpya kwa misimu miwili ya kipindi cha usajili majira ya kiangazi kutokana na kukiuka mkataba huo. Pia mchezaji huyo naye alifungiwa kucheza mechi yoyote kwa kipindi cha miezi minne huku tayari akiwa ameshatumikia miezi mitatu kwenye adhabu hiyo.
No comments:
Post a Comment