Tuesday, February 5, 2013

KAKA YAKE BERLUSCONI AINGIA MATATIZONI KWA KAULI YA KIBAGUZI.

MAKAMU wa rais wa klabu ya AC Milan, Paolo Berlusconi ameiingiza klabu hiyo katika kikaango baada ya kutoa zinazoashiria ubaguzi wakati akimtambulisha mshambuliaji nyota alisajili karibuni Mario Balotelli. Picha za video zilizoonyeshwa katika vyombo vya habari vya Italia vilimuonyesha Berlusconi ambaye ni kaka yake na rais wa klabu hiyo aliyewahi pia kuwa Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi akitoa kauli hiyo wakati akiwa katika kikundi cha watu wengi wao wakiwa marafiki zake. Katika picha za video zilizotolewa Berlusconi alisikika akiwaambia watu hao kuwa waende uwanjani kumuangalia kijana mdogo mweusi mwenye wazimu kichwani kwenye familia yao. Vyombo vya habari nchini Italia vilidai kuwa Berlusconi alitoa kauli hiyo mwishoni mwa mkutano wa kisiasa uliofanyika Varedo karibu na jiji la Milan. Balotelli ambaye alisajiliwa na Milan akitokea klabu ya Manchester City wiki iliyopita, alianza vyema kuitumikia klabu hiyo baada ya kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa mabao 2-1 timu yake iliyopata dhidi ya Udinese. 

No comments:

Post a Comment