Tuesday, February 12, 2013
FEDERER ATAKA PASI ZA KIBAOLOGIA KATIKA TENISI.
MCHEZAJI tenisi nyota kutoka Switzerland, Roger Federer amedai kuwepo na pasi za kibaologia kama zinazotumika katika mshindano ya baiskeli ili kugundua wachezaji wanaotumia dawa za kuongeza nguvu katika mchezo huo. Mchezaji huyo bingwa wa michuano ya Wimbledon alirudia madai yake kuwa hivi sasa wanafanyiwa vipimo vya damu mara chache kuliko kipindi wakati anaanza kucheza tenisi. Nyota hyo mwenye umri wa miaka 31 alidai kuwa utaratibu unatumika katika mashindano ya baiskeli unahitajika kwakuwa kuna viini vingine haviwezi kugunduliwa hivi sasa lakini pia kunahitajika vipimo zaidi vya damu ili kupambana na wadanganyifu. Mbali na Federer pia Novak Djokovic wa Serbia naye alilalamika kuwa kipindi cha mwaka jana vipimo vya damu walivyofanyiwa vilipungua tofauti na miaka iliyopita wakati Andy Murray wa Uingereza naye alidai kuongezwa kwa fedha zaidi kwa ajili ya kusimamia zoezi hilo la upimaji. Shirikisho la Kimataifa la Baiskeli lilitambulisha mfumo wa pasi za kibaologia mwaka 2008 ambapo huchukua vipimo vya damu na kuifananisha na damu halisi ya mwendesha baiskeli ili kugundua kama dalili zozote za kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment