Wednesday, February 6, 2013
GERRARD AMSIFU WILSHERE.
NAHODHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Steven Gerrard amemsifu kiungo nyota wan chi hiyo Jack Wilshere kuwa anaweza kuwa mchezaji mkubwa duniani baada ya kupona kabisa majeraha yaliyokuwa yakimsummbua. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 ameonyesha kiwango cha kuvutia toka aliporejea katika klabu yake ya Arsenal Octoba mwaka jana baada ya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi 15 kutokana na matatizo ya ifundo cha mguu. Mashabiki wa soka wa Uingereza wanamatumaini kuwa kiwango na ubunifu wa hali ya juu alionao nyota huyo linaweza kuwa jibu kwa kocha wa nchi hiyo Roy Hodgson ambapo Gerrard anakubaliana na hilo. Gerrard alithubutu kusema kuwa nyota huyo anaweza kufikia kiwango cha viungo nyota wa Hispania Andres Iniesta na Xavi Hernandez kutokana na uwezo wake wa kunyang’anya mpira, kuzunguka uwanja mzima, kutengeneza mabao na kufunga. Wilshere kwa mara kwanza aliichezea Uingereza Agosti mwaka 2010 na sasa anajipanga kucheza mchezo wake wa saba wa kimataifa akiwa na timu hiyo katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Brazil unaochezwa leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment