Wednesday, February 6, 2013

POLEKSIC AKANA TUHUMA ZA UAPNGAJI MATOKEO.

GOLIKIPA wa klabu ya Debrecen ya Hungary, Vukasin Poleksic amekataa tuhuma za kupanga matokeo katika wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool uliochezwa mwaka 2009 kwa kudai kuwa kiwango cha juu alichoonyesha kwenye mchezo huo ndio shahidi wake mkubwa. Polisi wa Ulaya wamesema kuwa wanazitilia shaka mechi zipatazo 680 zikiwemo mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia na Kombe la Ulaya pamoja na mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa vilabu vikubwa kwa kupanga matokeo. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kufungwa kwa Debrecen bao 1-0 na Liverpool kulitiliwa shaka kwamba ulikuwa ni mpango uliosukwa ya timu hiyo kutokubali nyavu zake kutikiswa mara zaidi ya mbili lakini klabu hiyo nayo ilikana tuhuma hizo. Golikipa huyo aliliambia gazeti la Daily Mail la Uingereza kuwa yoyote aliyetazama mchezo huo siku hiyo atajua kwamba tuhuma anazotupiwa ni zakuzusha kwani ulikuwa ni mchezo mkubwa toka aanze kusakata kabumbu hivyo haamini kama watu wanaweza kusema maneno kama hayo juu yake.

No comments:

Post a Comment