Sunday, February 17, 2013
KENYA YAJIPANGA KUOMBA KUANDAA AFCON 2019.
KENYA inajipanga kuwa nchi ya tatu kwa upande wa Afrika Mashariki baada ya Sudan na Ethiopia kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019. Shirikisho la Soka la Kenya-FKF limedokeza kuwa watatumia michuano ya Afrika ya Vijana watakayoandaa mwaka 2017 kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani humu. Katika taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo ilidai kuwa FKF kwa kushirikiana na Wizara ya Vijana na Michezo nchini humo wanajipanga ili kutuma maombi ya kuandaa michuano ya Afcon 2019 pamoja na ile ya vijana itakayofanyika mwaka 2017. Taarifa hiyo ilidai kuwa serikali kwa kupitia wizara hiyo tayari imetoa ruhusa kwa FKF kuomba kuandaa michuano hiyo na sasa wanakabiliwa na upinzani kwa Algeria, Nigeria, Liberia, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ambao nao wote wameomba kuandaa michuano ya kipindi hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment