Friday, February 1, 2013

KOCHA WA CAPE VERDE ATAMBA KUNYAKUWA AFCON.

KOCHA wa timu ya taifa ya Cape Verde, Lucio Antunes ametabiri kikosi chake kiyakuwa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon inayofanyika nchini Afrika Kusini mwaka huu. Cape Verde itaikabili Ghana katika mchezo wa Robo Fainali utakaochezwa katika Uwanja wa Port Elizabeth Jumamosi na kocha huyo anaamini kuwa kikosi chake kimeonyesha kiwango bora baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi A nyuma ya wenyeji Afrika Kusini kwa tofauti ya bao moja. Anmtunes amesema michuano ya mwaka huu inatofauti kubwa na michuano iliyopita na kuamini kuwa kikosi chake kinajiamini zaidi na kiko imara hivyo wana nafasi ya kusonga mbele mpaka katika hatua ya fainali ya michuano hiyo. Kocha huyo anasema bidii ndio silaha pekee itakayowawezesha kuwashangaza watu kwa kunyakuwa taji hilo kama walivyofanya Zambia mwaka jana.

No comments:

Post a Comment