Friday, February 1, 2013

GIBBS NJE WIKI SITA.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa beki wake wa kushoto Kieran Gibbs atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita kutokana na majeraha yanayomsumbua. Gibbs mwenye umri wa miaka 23 alilazimika kutoka katika kipindi cha kwanza baada ya kuumia paja wakati wa mchezo dhidi ya Liverpool ambao walitoka sare ya mabao 2-2. Wenger alithibitisha kuumia kwa nyota huyo baada ya kupata taarifa ya uchunguzi wake kutoka madaktari na sasa antegemea kumtumia Andre Santos kuziba nafasi hiyo. Pamoja na kumsajili beki mwingine wa nafasi hiyo Nacho Monreal kutoka klabu ya Malaga ya Hispania Wenger alionyesha bado kuwa na imani na Santos ambaye katika mchezo dhidi ya Liverpool alicheza chini ya kiwango. Wenger alimtetea santos akidai bado yuko katika kiwangi kizuri pamoja na makosa aliyofanya katika mchezo uliopita na kusema baadhi ya lawama anazotupia na mashabiki hastahili.

No comments:

Post a Comment