Friday, February 1, 2013

LANGALANGA 2013: FERRARI YAZINDUA GARI JIPYA.

TIMU ya Ferrari imezindua gari lake jipya litakalotumika kwa mwaka huu 2013 ili kujaribu kumaliza ukame wa vikombe latika mashindano ya Langalanga. Gari hilo aina ya F138 lilizinduliwa na kiongozi wa timu hiyo Stefano Domenicali akidai kuwa madhumuni makubwa ya kutumia gari ya aina ni kuweka historia ya kuvutia katika mashindano ya mwaka huu baada ya ukame wa miaka mingi. Mara ya mwisho Ferrari kushinda taji katika michuano hiyo ilikuwa ni mwaka 2008 wakati huo ikiendeshwa na dereva Kimi Raikkoen. Domenicali amedai kuwa wataanza msimu wa mwaka huu kiushindani zaidi katika mbio zitafanyika jijini Melbopurne, Australia tofauti na mbio za msimu uliopita ambapo walianza vibaya. Mwaka jana walilikosa taji hilo na kukamata nafasi ya pili baada ya Sebastian Vettel timu ya Red Bull kufanikiwa kushinda taji hilo kwa tofauti ya alama tatu pekee mbele ya Fernando Alonso ambaye amehamia timu ya Marcedes mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment