Monday, February 11, 2013
MAISHA YA GAZZA HAYAKO HATARINI - DAKTARI.
DAKTARI wa ushauri anayemtibu Paul Gascoigne maarufu kama Gazza amesema hakuna hofu yoyote ya kupoteza maisha kwa nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza baada ya kupelekwa wodi ya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu nchini Marekani. Gazza mwenye umri wa miaka 45 aliwahishwa hospitali baada ya kupata maambukizi mabaya wakati akiwa jijini Arizona alipokuwa akipatiwa matibabu ya kupambana na tatizo la ulevi uliopindukia alilonalo. Lakini daktari wake wa muda mrefu anayemtibu tatizo hilo John McKeown aliwahakikishia kuwa maisha ya Gazza hayako katika hatari yoyote kwani ameamka na anaweza kutembea mwenyewe baada ya kupatiwa matibabu. McKeown ambaye amefanya kazi na Gazza kwa zaidi ya miaka 10 alidai kuwa baadhi ya dawa alizopewa nyota huyo kwa ajili matibabu ya ulevi hazikuendana naye ndio maana zikamletea matatizo hayo. Lakini daktari huyo alidai kuwa hilo sio suala la kushangaza kwa mtu aliyekuwa anakunywa kupindukia kama Gazza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment