Saturday, February 9, 2013

BOLT AANZA MSIMU KWA KUSUASUA.

MWANARIADHA nyota wa mbio fupi, Usain Bolt kutoka Jamaica ameshindwa kutamba katika mashindano ya kwanza aliyoshiriki msimu huu kwa kumaliza katika nafasi ya tatu katika mbio za mita 400 zilizofanyika jijini Kingston. Bolt ambaye ni bingwa wa medali tatu za dhahabu katika michuano ya olimpiki ya Beijing mwaka 2008 na London 2012 alishinda heat yake kirahisi katika mbio hizo za Camperdown Classic akitumia muda wa sekunde 46.71. Lakini katika heat ya mwisho ambayo iliwashirikisha wanariadha Warren Weir na Yohan Blake ilishuhudia wanariadha hao wakitumia muda wa haraka zaidi baada ya Weir kushinda heat hiyo kwa kutumia muda wa 46.23 huku Blake akishika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa sekunde 46.64. Pamoja na kushindwa kufanya vyema katika mbio hizo lakini Bolt amesema anafurahi amemaliza salama bila kuwa na majeraha yoyote hivyo muda siyo tatizo sana kwake kwani bado wana msimu mrefu.

No comments:

Post a Comment