Friday, February 15, 2013
MARUFUKU MASHABIKI WA CROATIA NA SERBIA KUSAFIRI KUZISJANGILIA TIMU ZAO.
NCHI za Croatia na Serbia zimeafikiana kuwazuia mashabiki wake kwenda kushangilia mechi za ugenini wakati timu hizo zitakapokutana katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Mashirikisho ya soka ya nchi hizo mbili yalifikia uamuzi huo ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokea wakati nchi hizo zitakapokutana katika mechi mbili moja ikichezwa jijini Zagreb na na nyingine Belgrade. Katika taarifa yao ya pamoja ilidai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kunaweza kutokea madhara makubwa kama wakiruhusu mashabiki wan chi zote mbili kukutana katika mechi hizo mbili za kundi A. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukikuwa toka mwaka 1990 baada ya kujitenga kwa kwa Croatia kwa Yugoslavia ya zamani ambayo nayo baadae ilikuja kujimega na kupatikana nchi za Montenegro na Serbia. Toka kipindi hicho maofisa wa soka wanaamini kuwa kuwakutanisha mashabiki wa pande hizo mbili usalama unaweza kuwa mdogo kutokana na chuki ambayo bado imeendelea kuwepo baina ya wananchi wan chi hizo. Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchea Machi 22 mwaka huu jijini Zagreb wakati mchezo mwingine wa marudiano utachezwa Septemba 6 jijini Belgrade.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment