Friday, February 15, 2013
MASHABIKI WA LIVERPOOL WASHAMBULIWA URUSI.
VYOMBO vya habari nchini Urusi vimeripoti kuwa mashabiki wa soka wa klabu ya Liverpool walishambuliwa na kikundi cha wahuni kabla ya mchezo wao wa kwanza wa Europa League dhidi ya Zenit St Petersburg. Taarifa iliyotolewa ilidai kuwa Jumatano jioni kikundi cha wahuni waliofikia kama watu 40 walilivamia kundi dogo la mashabiki wa Liverpool waliokuwa wametoka bar hali iliyopelekea mashabiki hao kurudi tena walipotoka ili kujaribu kujilinda. Watu wa usalama waliokuwepo katika bar hiyo walifanikiwa kulidhibiti kundi la wahuni hao kabla ya kuwasindikiza mashabiki wapatao saba wa Liverpool kwenda sehemu ya usalama na kuna taarifa kuwa hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Zenit iliihakikishia Liverpool juzi kuwa mashabiki watakaohudhuria mchezo kati ya timu hizo watakuwa salama baada ya kuzuka wasiwasi kuhusu suala la ubaguzi. Mashabiki wa Zenit ndio wamekuwa gumzo kutokana na tabia yao ya ubaguzi wa rangi wa waziwazi baada ya Desemba mwaka jana baadhi yao kutaka klabu hiyo kutosajili wachezaji weusi ili kutoa nafasi zaidi kwa wachezaji wa nyumbani au Ulaya kwenye timu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment