Friday, February 15, 2013

PISTORIUS AFIKISHWA KOTRINI.

MWANARIADHA nyota mlemavu Oscar Pistorius wa Afrika Kusini, amefikishwa mahakamani akikabiliwa kwa madai ya kumuua mchumba wake kwa kumpiga risasi nyumbani kwake mjini Pretoria, Afrika Kusini. Pistorius alitiwa nguvuni toka jana kutokana na tuhuma hizo katika kituo cha polisi na uamuzi utaafikiwa ikiwa ataruhusiwa kupewa dhamana lakini anakabiliwa na wakati mgumu kwani waendesha mashtaka wanataka Pistorius aendelee kubakia lupango. Mwandishi wa BBC Andrew Harding, mjini Pretoria, amesema kuwa maelezo fulani, ya kesi hiyo dhidi ya Pistorius mwenye umri wa miaka 26 na upande wa utetezi yatatolewa baadaye leo. Wataalamu wa uchunguzi, wanatarajiwa kuendelea na uchunguzi wao katika nyumba ya Pistorius ambako mchumba wake Steenkamp, aliuawa. Duru zinasema kukamatwa kwa Pistorous kumewashangaza wengi sana Afrika Kusini ambako anatazamiwa kama shujaa. Pistorius alikuwa mkimbiaji wa kwanza mlemavu kuruhusiwa na shirika la kimataifa la riadha kuweza kushindana na wanaridha wengine wasio na ulemavu wowote.

No comments:

Post a Comment