KIUNGO nyota wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa, Andre Ayew ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ya klabu hiyo lakini nyota huyo amedai bado ana nafasi kubwa ya kukuza kipaji chake huko mbele. Klabu hiyo imecheza mechi tatu mwezi huu wa pili na mashabiki wametoa asilimia 55 ya kura zao walizopiga kwa kiungo huyo kwa kiwango cha hali ya juu alichokionyesha mwezi uliopita. Nyota huyo aliwashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa imai kubwa waliyoonyesha kwake na kuahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi huko mbele baada ya kupona majeraha ambayo yalikuwa yamemuandama katika siku za karibuni. Katika kura hizo mdogo wake Andre aitwae Jordan ambaye wanacheza wote kwenye klabu hiyo alishika nafasi ya pili katika kura hizo kwa kupata asilimia 24.
No comments:
Post a Comment