Thursday, February 7, 2013
MECHI ZA KIMATAIFA ZAMUACHIA MAJANGA WENGER.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameachwa akijutia mzunguko wa mechi za kimataifa zilizofanyika katikati ya wiki baada ya baadhi ya wachezaji wake waliokuwa na timu zao taifa kupata majeraha. Wenger anaweza kuwakosa nyota wake Laerent Koscielny, Aaron Ramsey na Theo Walcott katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza Jumamosi dhidi ya Sunderland baada ya nyota hao kupata majeraha wakati wakitumikia timu zao za taifa. Koscielny ambaye ni beki wa kati wa timu ya taifa ya Ufaransa alilazimika kutolewa nje katika mchezo ambao timu yake ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ujerumani wakati Ramsey ambaye ni kiungo wa timu ya taifa ya Wales naye alienguliwa kwenye kikosi cha nchi hiyo kabla ya mchezo wao na Austria kwa matatizo ya msuli. Walcott alicheza dakika 76 katika mchezo ambao Uingereza ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Brazil kabla ya kumpisha Aaron Lennon kuchukua nafasi yake lakini kulikuwa na taarifa kuwa nyota huyo alionekana kuchechemea baada ya mechi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment