Wednesday, February 13, 2013
MIELEKA KUONDOLEWA MICHUANO YA OLIMPIKI 2020.
KAMATI ya Kimataifa ya Olimpiki inapanga kuondoa mchezo wa mieleka katika michuano ya mwaka 2020 ikiwa ni katika harakati za kuingiza mchezo mwingine mpya. Kamati hiyo ilipendekeza kuondoa mchezo huo baada ya kufanyia tathmini michezo yote 26 iliyokuwepo katika michuano ya olimpiki iliyofanyika London mwaka jana. Ofisa Mkuu wa Chama cha Mieleka nchini Uingereza, Colin Nicholson amesema taarifa hizo za IOC zinakatisha tamaa hususani kwa wapenzi na wachezaji wa mchezo huo duniani. Kuna uwezekano mdogo sana mchezo huo wa mieleka kushinda wakati IOC watakapofanya mkutano Septemba mwaka huu ili kutoa maamuzi ya mwisho. Michezo ambayo ilidhaniwa kuwa katika hatari ya kupendekezwa kuondolewa kwenye michuano hiyo katika mkutano wa IOC uliofanyika jana jijini Lausanne, Switzerland ilikuwa ni pentathlon na taekwondo lakini cha kushangaza mchezo wa mieleka ndio ukapendekezwa. Katika mkutano huo wa Septemba IOC pia itaamua ni mji gani kati ya Istabul, Madrid au Tokyo itapewa uenyeji wa kuandaa michuano ya olimpiki 2020.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment